KAZI kubwa inapaswa kufanyika kwenye anga la kimataifa kwa wawakilishi wetu kufanya kweli kwenye kusaka matokeo.
Kila timu inatambua kwamba ushindani ni mkubwa hivyo muhimu kujituma bila kuchoka katika kutimiza majukumu ndani ya dakika 90.
Malengo ya msimu uliopita ni muhimu kuyatazama na kujua ni wapi yalipoishia kisha kuanza upya pale ambapo yalikwama kwenda sawa ili kuendelea kuwa imara zaidi kwa msimu mwingine katika anga la kimataifa.
Hakuna muda wa kuanza kulaumiana kwa sasa zaidi ni kufanyia kazi makosa ili kuendelea kusonga mbele kwa ajili ya wakati ujao ambao utakuwa bora zaidi.
Muda hausubiri kwenye anga la kitaifa na kimataifa vitu vinakwenda kasi na hakuna suala la kusubiri kitakachotokea bali ni lazima kujipanga kwa ajili ya kupata kile ambacho kinatakiwa kwenye kila idara.
Ugenini ilikuwa kazi kubwa ya kwanza ambayo hitimisho lake itakuwa nyumbani kwa timu ambazo zinashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.
Ushindani umekuwa mkubwa na kila timu inapambana kufanya kweli katika mechi ambazo ni ngumu. Hakunahttps://bit.ly/3CuDAzI kukata tamaa ni muhimu kuendelea kupambana mpaka mwisho.
Picha kamili inakwenda kupatikana kwenye mechi zinazitarajiwa kuchezwa hivi karibuni. Hapo kila kitu kitakuwa wazi baada ya dakika 90 kukamilika muhimu ni kuwa makini kwenye matumizi ya nafasi zitakazopatikana.
Iwe nyumbani ama ugenini kitu cha msingi ni kupambana kwa umakini na kupata matokeo mazuri hilo litaongeza nguvu ya kujiamini na kupata matokeo mazuri kwenye mechi zinazofuata.
Kwenye Kombe la Shirikisho Singida Fountain Gate kete yao ilianza nyumbani hivyo kazi ugenini itakuwa kukamilisha ngwe ya kwanza iliyoanza hapa nyumbani na inawezekana kupata ushindi ugenini.
Maandalizi mazuri kwenye kila hatua kuanzia benchi la ufundi na wachezaji wenyewe kujituma pale watakapopewa nafasi ya kuanza kwa kuwa haya mashindano ya kimataifa ni kwa ajili ya taifa kiujumla.
Muhimu kila mmoja kuhakikisha anatimiza wajibu wake kwa umakini na muda uliopo ni sasa hakuna ambaye anapenda kupata matokeo mabaya.
Pia ni muhimu wachezaji kuongeza nidhamu wawapo eneo la mafunzo na wakiwa nje ni muhimu kwa ajili ya kuendeleza viwango vyao.
Nidhamu ni kitu cha muhimu katika kutimiza majukumu yote na inaongeza uelewa hata pale ambapo mchezaji anakuwa hajaelewa inakuwa rahisi kwa benchi la ufundi kumpa mbinu nyingine zaidi.
Mashabiki wanapenda kuona matokeo mazuri kwenye mechi zote hivyo wachezaji ni muhimu kuendelea kulitambua hilo na kulifanyia kazi.
Kila mmoja afanye kazi yake kwa umakini na kuhakikisha kwamba bendera ya Tanzania inapeperushwa vema iwe nyumbani ama ugenini ndani ya mechi za kimataifa.
Muda ni sasa kufanya maandalizi mazuri tunaamini kwamba matokeo ya mechi hizi muhimu za kimataifa yatatoa picha ya kile kinachofuata baada ya mechi kugota mwisho.