SINGIDA BIG DAY NI BIG KWELIKWELI, BASI JIPYA KUTOKA NBC

SINGIDA Fountain Gate hawataki mchezo kuanza msimu mpya na bonge moja ya basi mpya kabisa.

Ikumbukwe kwamba Agosti 2 2023 ni Singida Big Day Uwanja wa Liti mbali na kutambulishwa kwa kikosi kipya wametambulisha na basi jipya pia

Singida Fountain Gate msimu wa 2023/24 inaipeperusha bendera anga la kimataifa katika Kombe la Shirikisho Afrika.

Ni kutoka kwa wadhamini wa Ligi Kuu Bara NBC wamewakabidhi Singida Fountain Gate.

Shughuli ya kukabidhiwa basi jipya la Singida Fountain Gate imefanyika Uwanja wa Liti.

Singida Fountain Gate inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya AS Vita kutoka DR Congo.

Timu hiyo iligotea nafasi ya nne kwenye ligi msimu wa 2022/23 imesajili wachezaji wapya ikiwa ni pamoja na Joash Onyango, Yahya Mbegu ipo na wachezaji wengine walikuwa na kikosi hicho msimu uliopita.

Ni Meddie Kagere, Deus Kaseke, Bruno Gomes walikuwa na kikosi cha Singida Fountain Gate msimu wa 2022/23.