TIMU ya Chelsea leo imeonja joto ya jiwe kwa kuchapwa mabao 3-2 dhidi ya West Ham United.
Licha ya Thiago Silva kuanza kupachika bao dakika ya 28 halikuweza kuwatoa kwenye reli West Ham kwa kuwa waliweka usawa dakika ya 40 kupitia kwa Manuel Lanzini ambaye alifunga kwa mkwaju wa penalti.
Chelsea ilitumia dakika nne kuandika bao lao la pili kupitia kwa Mason Mount dakika ya 44 na kuwafanya wakamilishe dakika 45 za mwanzo wakiwa mbele kwa mabao hayo mawili.
Dakika ya 56 Jarrod alipachika bao la pili kwa West Ham na lile la ushindi lilifungwa na Masuaku dakika ya 87 na kuwafanya Chelsea kupoteza pointi tatu mazima.