AZAM FC YAITULIZA COASTAL UNION, MBOMBO ATUPIA

IDRIS Mbombo nyota wa Azam FC amefikisha bao lake la 8 Uwanja wa Mkwakwani wakisepa na pointi tatu dhidi ya Coastal Union.

Katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa leo ubao umesoma Coastal Union 0-2 Azam FC.

Mbombo alitupia kambani bao la kuongoza dakika ya 58 ambalo liliwaongezea nguvu Azam FC.

Kwenye mchezo huo dakika 45 za mwanzo zilikamilika bila timu hizo kufungana.

Ni Prince Dube wa Azam FC alipachika bao dakika ya 90 likiwa ni bao la ushindi kwa Azam FC.