Home International YANGA WAANIKA MBINU WATAKAZOTUMIA KUWAMALIZA WAARABU

YANGA WAANIKA MBINU WATAKAZOTUMIA KUWAMALIZA WAARABU

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa utatumia mbinu kama walizotumia kuwatuliza Waarabu wa Tunisia Club Africain kwenye mchezo wao dhidi ya USM Alger Waarabu wa Algeria.

Leo Juni 3, Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ina kibarua cha kusaka ushindi baada ya kushuhudia Uwanja wa Mkapa ukisoma Yanga 1-2 USM Alger bao la Yanga likifungwa na Fiston Mayele.

Ikumbukwe kwamba Novemba 9 Yanga ilishuhudia ubao wa Uwanja Olympiques de Rades ukisoma Club Africain 0-1 Yanga kwenye mchezo wa hatua ya mtoano.

Bao pekee la ushindi lilifungwa na Aziz KI dakika ya 79 kwa mguu wake wa kushoto akiwa nje ya 18 na kuifanya Yanga kusonga mbele mpaka hatua ya makundi.

Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Yanga 0-0 Club Africain.

 Ally Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wanatambua namna ya kucheza mechi za ugenini na bado hawajakata tamaa.

“Labda watu wanasahau kwamba walipokuwa wametukatia tamaa kwenye mchezo wetu dhidi ya Club Africain walidhani mwisho wetu umefika lakini ilikwenda kuwa tofauti na tunaimani hiyo.

“Kama ambavyo hawakuamini tupopata ushindi ugenini kwa Club Africain tunakwenda kufanya kazi nyingine kwa mara nyingine kwa ajili ya Tanzania,” amesema Kamwe.

Previous articleSIMBA WAJA NA GIA NYINGINE
Next articleNAMUNGO FC WAPIGA HESABU KUMALIZANA NA DODOMA JIJI