KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema kuwa ni muhimu kwa safu yake ya ulinzi kuongeza umakini kwenye mapigo huru na mpira ya juu.
Ni Dickson Job ambaye ni beki chaguo la kwanza, Yannick Bangala huyu ni kiraka, Ibraham Bacca hawa Nabi hupenda kuwatumia kwenye eneo la ulinzi.
Leo Yanga ina kibarua cha kusaka ushindi dhidi ya Gallats Marumo mchezo wa hatua ya robo fainali Kombe la Shirikisho Afrika na ule wa marudiano unatarajiwa kuchezwa Mei 17,Afrika Kusini.
Nabi amesema kuwa wanatambua umuhimu wa kila mchezo kwenye mechi za kimataifa jambo wanalochukulia kwa umakini.
“Kila mchezo kwetu ni muhimu na ambacho tunahitaji ni ushindi na kupunguza makosa kwenye mipira ile ya juu pamoja na adhabu ambayo ni sababu kwetu kufungwa kwani mchezo ni mpira wa makosa.
“Tunachokifanyia kazi kwenye uwanja wa mazoezi ni yale makosa ambayo yamekuwa yakitokea ikiwa ni kwenye mipira ya adhabu katika kuokoa hivyo lazima kila mmoja awe makini katika kutimiza kazi yake,” amesema Nabi.
Tottenham Hotspur forward Dominic Solanke battles with Crystal Palace defender Maxence Lacroix during the English championship Premier League football match between Crystal Palace and Tottenham Hotspur on 27 October 2024 at Selhurst Park in London, England - Photo Ian Stephen / ProSportsImages / DPPI (Photo by IAN STEPHEN / ProSportsImages / DPPI via AFP)