KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi ameweka wazi kuwa wapinzani wao Marumo Gallants atakaokutana nao kwenye hatua ya nusu fainali sio wabaya ni timu nzuri.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa na tayari wapinzani wao Gallants wamewasili Bongo alfajiri ya leo.
Nabi amesema kuwa wanatambua umuhimu wa mchezo huo wa kesho na mahitaji makubwa ni kupata matokeo ili kusonga mbele hatua ya fainali.
“Marumo ni timu nzuri, na sisi tunajiandaa kucheza na timu iliyofika hatua ya nusu fainali hivyo tupo tayari na tunawakaribisha Tanzania.
“Kikubwa ni kwa mashabiki ambao watajitokeza ni kuona wanashangilia uwanjani mwanzo mwisho kuanzia dakika ya kwanza mpaka ile ya 90 hii itawaongezea nguvu wachezaji kupambana,” amesema.
Miongoni mwa wachezaji ambao wapo kambini kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo huo ni Aziz KI mwenye tuzo ya mchezaji bora Mei, Jesus Moloko, Fiston Mayele, Kibwana Shomari, Djigui Diarra, Khalid Aucho, Khalid Aucho na Morrison.
Tottenham Hotspur forward Dominic Solanke battles with Crystal Palace defender Maxence Lacroix during the English championship Premier League football match between Crystal Palace and Tottenham Hotspur on 27 October 2024 at Selhurst Park in London, England - Photo Ian Stephen / ProSportsImages / DPPI (Photo by IAN STEPHEN / ProSportsImages / DPPI via AFP)