JULIO AKABIDHIWA WANA KINO BOYS

JAMHURI Kihwelo,’Julio’ atakuwa ndani ya KMC kwenye mechi nne ambazo zimebaki msimu wa 2022/23.

Ni Hitimana Thiery alikuwa anakiogoza kikosi hicho mkataba wake umevunjwa baada ya makubaliano ya pande zote.

Yote hayo yalifanyika Aprili 13,2023 ambapo tayari Julio ametambulishwa kwa ajili ya kuwanoa Wanakino Boys.

Mchezo wa mwisho Hitimana kukiongoza kikosi cha KMC alishuhudia ubao wa Uwanja wa Uhuru ukisoma KMC 0-2 Geita Gold.

Kwenye msimamo KMC ipo nafasi ya 14 pointi 26 baada ya kucheza mechi 26.