YANGA YAINGIA ANGA ZA MSHAMBULIAJI HUYU MATATA

 

IMEELEZWA kuwa mshambuliaji namba moja ndani ya kikosi cha Mbeya Kwanza, Chrispin Ngush jina lake limependekezwa na Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi aweze kusajiliwa.

Inatajwa kwamba kamati ya Usajili ya Yanga nayo pia haijapinga hoja hiyo na badala yake imeweka watu maalumu kwa ajili ya kumfuatilia nyota huyo

Ngushi ni kinara wa mabao ndani ya Mbeya Kwanza akiwa nayo matatu na moja ni lile kali alilowafunga Mveya City alilowatungua kwa mtindo wa kubinuka, ‘Acrobatic ‘ ambalo linatajwa kuwa bora zaidi.

Dirisha la Usajili Bongo linatarajiwa kufunguliwa Desemba 15 mwaka huu na litahusisha timu za Ligi Kuu Bara, Championship na First League.