>

KOCHA SIMBA ANAAMINI VIWANGO VINAZIDI KUPANDA

KOCHA Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira amesema kuwa maendeleo ya wachezaji wake pamoja na viwango vyao vinazidi kuwa imara kila siku.

Kocha huyo raia wa Brazil amebainisha kuwa anafurahishwa na uwezo wa kila mchezaji kwa namna anavyojituma kwenye kikosi.

Ijumaa wachezaji wa Simba walianza mazoezi kwa ajili ya mchezo wao ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca.

“Wachezaji wanafanya kazi kubwa na kila siku viwango vyao vinaongezeka katika hilo ninawapongeza na ninaamini tutazidi kuwa imara.

“Mchezo wetu uliopita tulipata ushindi dhidi ya Horoya kwa kufunga mabao mengi na kupata pointi tatu hili ni jambo zuri na kubwa kwetu tunaamini imetuongezea hali ya kujiamini,”

Miongoni mwa wachezaji ambao walianza mazoezi Ijumaa ni pamoja na Mohamed Hussein, Kibu Dennis, Shomari Kapombe, John Bocco.