TANZANIA PRISONS YAGOMEA KUSHUKA DARAJA

MOHAMED Abdalaha, ‘Bares’ Kocha Mkuu wa Tanzania Prisons amesema kuwa mashabiki wawe na Imani timu hiyo haitashuka daraja licha ya presha ambayo wanaipitia pamoja na mwendo ambao hawaufurahii.

Mchezo wao uliopita Uwanja wa Majaliwa ulisoma Namungo 2-3 Tanzania Prisons na kuwafanya wasepe na pointi tatu ugenini.

Haikuwa kwenye mwendo mzuri katika mechi zake za hivi karibuni Februari 25 ilishuhudia ubao wa Uwanja wa Mkwakwani ukisoma Coastal Union 1-0 Prisons mchezo wa ligi na iliondolewa hatua ya 16 bora na Yanga Machi 3,2023 Kombe la Azam Sports Federation kwa kufungwa mabao 4-1 Uwanja wa Azam Complex.

Bares amesema:”Unaona timu inacheza na wachezaji wana presha kubwa ya kupata matokeo mazuri hilo linawafanya wapambane na wanaonyesha uwezo mkubwa hivyo bado tuna nafasi ya kubaki kwenye ligi.

“Ninachoweza kuwaambia mashabiki ni kwamba wawe na Imani tuna amini tutabaki kwenye ligi kwani mechi zipo na pointi 25 ambazo tunazo sio haba muhimu ni kupambana kwani huu ni mpira na kila kitu kinawezekana,” .

Kwenye msimamo ipo nafasi ya 13 ikiwa imecheza mechi 25 ikiwa na wastani wa kukusanya pointi moja kwenye kila mchezo.