Home Sports KIUNGO WA KAZI AREJEA NDANI YA KIKOSI CHA SIMBA

KIUNGO WA KAZI AREJEA NDANI YA KIKOSI CHA SIMBA

KIUNGO wa kazi ndani ya Simba, Hassan Dilunga amerejea kwenye uwanja wa mazoezi baada ya kuwa nje kwa muda mrefu akipambania afya yake.

Nyota huyo aliumia kwenye mazoezi wakati timu hiyo ilipokuwa kwenye maandalizi ya mechi zake za ushindani.

Taarifa iliyotolewa na Simba imeeleza kuwa HD amerejea ndani ya kikosi hicho baada ya kupona.

Hivi karibuni Dilunga aliweka wazi kuwa ado hajaachana na Simba kwa kuwa hata suala la matibabu walikuwa wanagharamia.

Pia alibainisha kwamba licha ya kwamba hakuwepo kwenye utambulisho bado jezi yake namba 24 hakuna ambaye alipewa licha ya yeye kutokuwepo kwenye kikosi.

Kwa sasa Simba ipo kwenye maandalizi ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Jumamosi.

Previous articleTANZANIA PRISONS YAGOMEA KUSHUKA DARAJA
Next articleMATAJIRI WANUNUA MABAO YANGA, BEKI SIMBA AONDOLEWA KAMBINI