MABINGWA watetezi wa Kombe la Azan Sports Federation, Yanga wamepenya hatua ya robo fainali baada ya kupata ushindi leo Machi 3,2023.
Uwanja wa Azam Complex umesoma Yanga 4-1 Tanzania Prisons ambapo mabao yote yamefungwa kipindi cha pili.
Ni Bakari Mwamnyeto alifungua ukurasa wa mabao dakika ya 51 kisha likawekwa usawa na Jeremiah Juma dakika ya 61.
Ni Clement Mzize alitupia kambani mabao mawili dakika ya 70 na 88 na alikosa penalti dakika ya 90 huku bao lingine ni mali ya Aziz KI dakika ya 84 kwa mkwaju wa penalti.
Cedrick Kaze, kocha msaidizi wa Yanga amesema kuwa walitambua mchezo utakuwa mgumu hasa ukizingatia ni mchezo wa mtoano.