VIDEO:CAF AFRICAN SCHOOLS FOOTBALL CHAMPIONSHIP ZONAL QUALIFIERS

CAF African Schools Football Championship Zonal Qualifiers, Azam Complex Stadium DSM…
MICHUANO ya WANAFUNZI YA CECAFA INAPIGWA AZAM COMPLEX

Michuano ya mpira wa miguu ya wanafunzi wa Ukanda wa CECAFA imeanza tangu Ijumaa Februari 17, 2023 katika Viwanja vya Azam Complex nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Michuano hiyo ambayo Tanzania ni wenyeji inashirikisha timu 15 kutoka nchi nane na imeanza Ijumaa na itadumu kwa siku tatu hadi Jumapili Februari 19, 2023.

Global TV ndicho kituo pekee cha runinga ambacho kimepata idhini ya kurusha matangazo hayo moja kwa moja kutoka Viwanja vya Azam Compex.

Mitanange hiyo itakuwa inaanza asubuhi saa 3:00 hadi saa 9:00 Alasiri kwa siku tatu mfululizo.