HOROYA 1-0 SIMBA CAF KIMATAIFA

DAKIKA 45 za mwanzo zimemeguka kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi

Horoya 1-0 Simba bao ambalo limepachikwa ndani ya dakika 30 za kipindi cha mwanzo.

Ni Pape Nd’iaye mwamba mmoja kaenda hewani akiwa huru na kumtungua kipa Aishi Manula.

Kazi ni nzito kwa Simba kwa kuwa hakuna shambulizi kali ambalo wamelifanya huku wakiwatumia viungo zaidi ya wanne kwenye kikosi cha kwanza.

Ni Mzamiru Yassin, Sadio Kanoute, Pape Sakho, Ismail Sawadogo kwenye kazi ya kusaka ushindi.