RAIS wa Yanga, Eng Hersi Said ameitembelea Klabu ya Royal FC inayoshiriki Ligi daraja la tatu kwenye Umoja wa Falme za Kiarabu.
Mmoja wa wamiliki wa Royal FC, iliyoanzishwa mwaka huu, Ali Mohammed Bujsaim, miongoni mwa marefa wenye heshima kubwa duniani.
Refa huyo ana rekodi ya kuchezesha Fainali za Kombe la Dunia mara tatu [1994,1998,2022].
Ziara ya Rais wa Yanga kwenye Klabu hiyo ni kutengeneza mahusiano mazuri kwa ajili ya kusaidia vijana wa Kitanzania kupata fursa ya kucheza soka kwenye Umoja wa Falme za Kiarabu.
Tayari msafara wa Yanga ambao una kibarua cha kucheza na US Monastri Februari 11 Tunisia kimewasili salama kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo.