CLATOUS Chama mwamba wa Lusaka amejiunga na kikosi cha Simba kambini Dubai leo Januari 11,2023.
Kiungo huyo hakuwa na timu hiyo kwenye msafara wa awali kutoka Dar kwenda Dubai kwa kuwa alikuwa nyumbani kwao Zambia.
Timu hiyo ipo chini ya Kocha Mkuu, Robert Oliviera raia wa Brazil ambaye anashirikiana na Juma Mgunda ambaye ni mzawa.
Ndani ya kikosi cha Simba, Chama amefunga mabao matatu na kutoa pasi 11 za mabao msimu wa 2022/23.
Kikosi hicho kipo Dubai kwa mualiko maalumu wa Rais wa Heshima wa timu hiyo Mohamed Dewji, ‘Mo’.