BAADA ya kuvuliwa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi na kurejea Dar kikosi cha Simba kinatarajia kukwea pipa leo Januari 7,2022 kuelekea Dubai.
Kikosi hicho kwenye mechi mbili za hatua ya makundi ambapo kilikuwa kinasaka pointi sita kiliambulia pointi tatu.
Mchezo wa kwanza ubao wa Uwanja wa Amaan ulisoma Simba 0-1 Mlandege ambao wametinga hatua ya nusu fainali Kombe la Mapinduzi 2023.
Leo saa 9 alasiri kikosi kitasafiri kwa kutumia ndege ya shirika la ndege la Emirates kuelekea Dubai kwa ajili ya maandalizi ya mechi za ligi na kimataifa ikishiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.
Miongoni mwa wachezaji ambao walicheza Kombe la Mapinduzi 2023 ni pamoja na Kiu Dennis, Habib Kyombe na Legend, Jonas Mkude.
Kwa mujibu wa Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa wanakwenda kufanya maandalizi kwa ajili ya mechi zao zote.