Home Sports YANGA WAFANYA HAFLA NA MATAJI YAO,WAREJEA DAR

YANGA WAFANYA HAFLA NA MATAJI YAO,WAREJEA DAR

UONGOZI wa Yanga chini ya Rais Eng Hersi Said, Benchi la ufundi na wachezaji leo Januari 7 2023 wamemtembelea Mama Fatma Karume pamoja na wajumbe wa Bodi ya Wadhamini na kuwakabidhi makombe manne waliyoshinda mwaka 2022.

Hafla hiyo imefanyika nyumbani kwa Mama Fatma Karume, maeneo ya Maisara, Zanzibar 2023.

Kikosi cha Yanga kilikuwa Zanzibar kwa ajili ya Mapinduzi Cup 2023 ambapo Yanga ilikuwa inashiriki na kugotea hatua ya makundi.

Leo kikosi kimewasili Dar kwa ajili ya maandalizi ya mechi za ligi, Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa imetinga hatua ya makundi.

Miongoni mwa nyota ambao walikuwa kwenye msafara wa leo ni pamoja na Clement Mzize, Mudhathir Yahya, Eric Johora.

Previous articleSIMBA KUKWEA PIPA KUIBUKIA DUBAI
Next articleSIMBA YAKWEA PIPA, BANDA,NTIBANZOKIZA NDANI