MEZA YAPINDULIWA KIBABE KWA CHELSEA UGENINI

NYOTA Serge Aurier bao lake la kwanza akiwa na Nottingham Forest dakika ya 63 liliuzima mkwaju wa Raheem Sterling  dakika ya 16 na kuwafanya wasumbufu hao wa Premier League kupata sare ya kufungana  1-1 waliyostahili dhidi ya Chelsea.

 Mchezo huo ulichezwa  kwenye Uwanja wa City Ground.

 Forest waliingia uwanjani wakijua ushindi ungewaondoa kwenye eneo la kushushwa daraja lakini hawajaweza kutwaa zote tatu.

 Steve Cooper alifurahishwa na uchezaji bora wa kipindi cha pili ambao uliifanya timu yake kuambulia pointi muhimu.

 Kwa upande wa Chelsea, ushindi ungewafanya wasonge mbele hadi kufikia pointi tano kati ya nne za juu na walionekana vyema kufanya hivyo wakati Sterling alipowapatia bao la kuongoza kipindi cha kwanza.

 Lakini kikosi hicho cha Graham Potter kilitoa matokeo ya kutisha katika dakika 45 za pili ambapo Forest walirejea na kujiweka katika nafasi ya nane kwenye ligi kabla ya safari ya kutisha dhidi ya Manchester City siku ya Alhamisi.