BEKI wa kati wa Manchester City, Nathan Ake alifunga bao la ushindi kwa kichwa wakati timu hiyo ikiwachapa mabingwa watetezi Liverpool 3-2 katika mchezo wa kusisimua wa Kombe la Carabao.
Ushindi huo uliopatkana Uwanja wa Etihad unaipa nafasi City kuweza kutinga hatua ya robo fainali.
Licha ya kutocheza kwa mechi za ushindani kwa mwezi mmoja wakati wa mapumziko ya Kombe la Dunia, City na Liverpool zilirejea uwanjani kwa kasi kuwa huku Fabio Carvalho dakika ya 20 akisawazisha bao la kwanza la Erling Haaland aliyepachika dakika ya 10 katika mwanzo wa kutatanisha.
Riyad Mahrez aliirudisha City mbele dakika mbili baada ya mapumziko lakini ndani ya sekunde 47 Liverpool walisawazisha kupitia kwa Mohamed Salah dakika ya 48.
Lakini Ake asiyejulikana alitokea kwenye lango la nyuma na kufunga bao muhimu dakika ya 58 baada ya krosi ya Kevin De Bruyne aliyetoa pasi yake ya pili ya bao la usiku na kuwapeleka City nafasi ya kufuzu kwa robo fainali ya Kombe la Carabao.
City walipangwa kukutana na Southampton katika robo fainali baada ya ushindi wa Alhamisi na watasafiri kwenda St Mary’s Januari 10 au 11.
Liverpool nusura waruhusu bao bila kugusa mpira baada ya mpira kuanza, Haaland alichukua fursa ya kutokuwepo kwa Virgil van Dijk huku Joel Matip na Joe Gomez wakijitahidi kukabiliana na mshambuliaji wa City huku wakiweka safu ya juu.