>

HII HAPA RATIBA YA YANGA KIMATAIFA

KLABU ya Yanga kwenye hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika imedondokea kundi D ambalo lina timu nne ikiwa ni pamoja na wawakilishi hawa kutoka Tanzania.

Timu nyingine ambazo zipo kwenye Kundi D ni TP Mazembe, US Monastir na Real Bamako.

Ikumbukwe kwamba US Monastri wao waliwafungashia virago RS Berkane huku Mazembe wao waliwahi kukutana na Yanga mwaka 2016 kwenye Klabu Bingwa Afrika na Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Yanga 0-1 TP Mazembe walipocheza ugenini, Yanga ilipoteza kwa kufungwa mabao 3-1 hivyo kazi sio nyepesi.

Ni Februari 12 Yanga itakuwa ugenini kwenye mchezo dhidi ya Monastri kisha Februari 19 itakuwa Uwanja wa Mkapa dhidi ya TP Mazembe, Feb 26 itamenyana na Bamako ugenini, Machi 8 itamenyana na Bakamo Uwanja wa Mkapa, Machi 19 itakuwa dhidi ya Monastri Yanga itakuwa nyumbani.

Kigongo kingine itakuwa ugenini ni Aprili 2,2023 dhidi ya TP Mazeme ambapo Yanga itakuwa ugenini.