Home Uncategorized KOMBE LA SHIRIKISHO LIMEKUWA LA KIPEKEE, MZUNGUKO WA PILI HUU HAPA

KOMBE LA SHIRIKISHO LIMEKUWA LA KIPEKEE, MZUNGUKO WA PILI HUU HAPA

MOJA ya msimu wenye ushindani mkubwa ndani ya ligi ni pamoja na huu ambao unaendelea kwa sasa 2022/23 kutokana na timu kujipanga kufanya vizuri.

Benchi la ufundi, uongozi pamoja na mashabiki muda wa kujipanga kwa makosa ya mzunguko uliopita ni sasa na itasaidia kuwa kwenye ushindani mzuri.

Kinachowakasirisha mashabiki ni timu kushindwa kupata kile inachostahili kwa muda mrefu jambo linalowavunja moyo mashabiki.

Haina maana kwamba mashabiki hawajui kuhusu ushindani uliopo wanajua lakini ni muhimu kuwepo na furaha pia sio kila wakati huzuni.

Pale ambapo timu itashindwa kupata matokeo haina maana kwamba haikuwa inahitaji kushinda zaidi ni mbinu na makosa ambayo yamefanyika ndani ya uwanja.

Mchezo wa mpira unahitaji maandalizi mazuri na kila timu ambayo itafanya maandalizi mazuri ina uhakika wa kupata matokeo chanya.

Kwa wakati huu ambao upo ni muhimu kila timu kufanya maandalizi ili iweze kupata kile ambacho inastahili. Ni ushindi na hakuna jambo jingine ambalo linasubiriwa na mashabiki.

Ikiwa timu itaanza kwa kuyumba mwanzo wa mzunguko wa pili inatoa picha kwamba huko inakokwenda inakwenda kuanguka kutokana na kupoteza dira mapema.

Lakini pia zipo ambazo ziliwahi kuanza kwa anguko ila mwisho ukawa ni watofauti. Historia inaonyesha kwamba ambazo huwa zinasalia ndani ya ligi kama zikianza kwa kusuasua ni chache.

Ni muda mwingine ambao unakuja kwenye ligi, kila timu ina malengo yake ambayo imejiwekea hivyo ni muhimu kuwa na mwendelezo mzuri kwa zile ambazo zilianza kwa kupata matokeo mazuri.

Ambazo zilikwama kushinda kwenye mechi zao nao wanajukumu la kuanza kwa umakini kwenye mzunguko wa pili.

Muhimu kufanya maandalizi mazuri kwa wakati huu ili kuwa kwenye mwendo mzuri kwenye mechi za mzunguko wa pili.

Hamna nanmna ambayo unaweza kuifanya na ukamficha shabiki kuhusu uwezo wa mchezaji. Na mara nyingine huwa inatokeo bahati mbaya mazingira yanamkataa mchezaji.

Haina maana kwamba mchezaji mazingira yakimkataa basi hafai apewe zigo la lawama hapana ni lazima apewe muda na aendelee kuaminiwa ili aweze kuonyesha kile ambacho anacho.

Imani yangu ni kwamba benchi la ufundi ambalo lilitoa ripoti kuhusu aina ya wachezaji ambao wanahitaji mwisho wa siku wakapewa hivyo katika hilo ni muhimu kila mmoja kuendelea na mipango aliyopanga.

Mashabiki wamekuwa wakizifuatilia timu zao na kuona namna gani zinapata matokeo na kwa wakati huu kuna suala mwendelezo wa Kombe la Shirikisho na huku ni muhimu kuwekeza nguvu.

Pongezi kwa timu ambazo zimeanza kufanya maandalizi kwa ajili ya mechi za raundi ya pili kutokana na matokeo waliyopata.

Muda ni sasa kuanza kufanya maandalizi kwani masiaha ya mpira hakuna kutulia kila siku kazi zinaendelea katika mipango kazi.

Pongezi kwa wachezaji ambao wamekuwa kwenye mwendelezo mzuri wa kutimiza majukumu yao hili linawapa nguvu wale wengine ambao wanapenda kuwafuatilia.

Wachezaji wengine wanajifunza kutoka kwenu na kufanya yale ambayo mtakuwa mnafanya.

Wazawa nao nina amini kwamba ujio wa wageni wanaofanya kazi nao kwenye eneo moja kuna jambo wanajifunza hivyo ni lazima wafanyie kazi kwenye eneo la mazoezi.

Muda ni sasa wa kufanya kweli kwenye eneo la mazoezi pamoja na eneo la uwanja hii itafanya kila mmoja kuvuna kile ambacho amepanda.

Previous articleKITASA CHA KAZI KUPEWA MKATABA SIMBA
Next articleHII HAPA RATIBA YA YANGA KIMATAIFA