SAKA KUWAKABILI SENEGAL

NYOTA wa timu ya taifa ya England, Bukayo Saka anatarajiwa kuanza kikosi cha kwanza kwenye mchezo wa leo dhidi ya timu ya taifa ya Senegal.

Huu ni mcheza kwanza kwa timu hizi mbili kukutana kwenye Kombe la Dunia na rekodi zinaonyesha kuwa hawajawahi kumenyana hata kwenye mchezo wa kirafiki.

Ikumbukwe kwamba nyota huyo ambaye anakipiga ndani ya Klabu ya Arsenal kwenye mchezo dhidi ya Wales katika kundi B alipumzisha huku Phil Fode na Marcus Rasford walitupia kwenye mchezo.

Historia itaandikwa kwa mabingwa wa Afrika Senegal kusaka ushindi kwenye mchezo huo ambapo England wanapewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa hatua ya robo fainli, Kombe la Dunia Qatar.