>

SENEGAL YAMCHAPA QATAR 3-1

SENEGAL wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji Qatar kwenye mchezo wa makundi Kombe la Dunia.

Uwanja wa Al Thumana mbele ya mashabiki 41,797 ngoma imepigwa.

Mchezo mmoja uliokuwa na ushindani mkubwa huku kipanamba moja wa Senegal Mendy akifanya kazi kubwa kuokoa michomo langoni mwake.

Ni mabao ya B Dia dakika ya 41, F Diedhia dakika ya 48 na A Dieng dakika ya 84 yalitosha kuipa ushindi Senegal.

Bao pekee la wenyeji Qatar na likiwa ni bao pekee kwenye mechi mbili ambazo wamecheza limefungwa na M. Muntari dakika ya 78.

Legend, Jay Jay Okocha amesema kuwa moja ya mchezo mzuri na uliokuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote.

“Ulikuwa ni mchezo mzuri na kila timu ilikuwa inapambana kusaka matokeo mwisho bahati imekuwa kwa Senegal.”.