>

MANE NDO BASI TENA QATAR

STAA wa Senegal, Sadio Mane ambaye anakipiga ndani ya Bayern Munich jitihada za kumrejesha kwenye ubora zimegonga mwamba.

Ni rasmi kuwa winga huyo mwenye kipaji cha kweli hatakuwa kwenye orodha ya wachezaji watakaocheza michuano ya Kombe la Dunia, Qatar.

Sababu kubwa ni majeraha ya mguu ambayo aliyapata akiwa na timu yake ya Bayern Munich hivi karibuni.

Taarifa ambayo ilitolewa na uongozi wa timu ya Senegal imebainisha kuwa Mane hatukuwepo kwenye fainali hizo ambazo zinatarajiwa kuanza kufanyika kesho Novemba 20,Qatar..

Mane alipata maumivu ya mguu wakati timu yake ikicheza mchezo wa Bundesliga dhidi ya Werder Bremen.