KIKOSI cha Yanga kimewasili salama Dar leo Oktoba 17.2022 kikitokea Sudan ambapo kilikuwa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Al Hilal.
Mchezo huo ulichezwa jana Oktoba 16,2022 na Yanga ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na kufanya ikwame kutinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kwa matokeo hayo Yanga itashiriki Kombe la Shirikisho Afrika kwa msimu wa 2022/23 hivyo bado ina kibarua cha kuipeperusha bendera ya kimataifa.
Nyota wa Yanga, Fiston Mayele amesema kuwa matokeo ambayo wameyapata yamewaumiza lakini watafanya vizuri kwenye mechi zao zijazo.
“Tumeumia kupoteza mchezo wetu na kushindwa kufikia malengo ya kutinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika tutafanya vizuri kwa mechi zijazo za kimataifa,” .