ARSENAL IPO KWENYE UBORA WAKE

ARSENAL inazidi kujiimarisha kwenye nafasi ya kwanza baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Liverpool na kuifanya kuwa kwenye ubora wake chini ya Kocha Mkuu, Mikel Arteta.

Uwanja wa Emirates mapema kabisa katika dakika ya kwanza Gabriel Martinelli kisha misumari miwili ilipachikwa na Bukayo Saka dakika ya 45 na dakika ya 76 kwa mkwaju wa penalti.

Mabao ya Liverpool ambayo haijawa kwenye mwendo bora msimu huu yalifungwa na Darwin Nunez dakika ya 34 na Roberto Firmino dakika ya 53.

Arsenal inafikisha pointi 23 ikiwa nafasi ya kwanza na ilipiga jumla ya mashuti 11 na 7 yalilenga lango huku Liverpool ambayo ipo nafasi ya 10 na pointi 10 ilipiga mashuti 8 na matatu yalilenga lango.