ARSENAL wamerejea tena juu walipokuwa mwanzo kabisa wa msimu baada ya ushindi wa mabao 0-3 ugenini dhidi ya timu ngumu ya Brentford.
Arsenal ilipachika mabao mawili kwa nyota wake William Saliba dakika ya 17 na Gabriel Jesus dakika ya 28 wote wakipachika mabao hayo kwa kutumia kichwa.
Bao jingine lilipachikwa na nyota Fabio Viera ambaye alipachika kwa shuti akiwa nje ya 18 na kuwafanya washinde mchezo huo mazima ilikuwa dakika ya 49.
Sasa Arsenal inafikisha pointi 18 baada ya kucheza mechi 7 ikiwa namba moja inafuatiwa na Man City iliyo nafasi ya pili na pointi 17 nayo imecheza mechi 7 ndani ya Ligi Kuu England.
Tottenham Hotspur forward Dominic Solanke battles with Crystal Palace defender Maxence Lacroix during the English championship Premier League football match between Crystal Palace and Tottenham Hotspur on 27 October 2024 at Selhurst Park in London, England - Photo Ian Stephen / ProSportsImages / DPPI (Photo by IAN STEPHEN / ProSportsImages / DPPI via AFP)