Simanzi Argentina! Mchezaji Mwenye Miaka 18 Afariki Baada Ya Kupigwa Teke La Kichwa

Mchezaji chipukizi wa soka kutoka Argentina, Abel Núñez (18), amefariki dunia baada ya kupata jeraha kubwa la kichwa kufuatia tukio la kupigwa teke la kichwa wakati wa mchezo kati ya FC Ezeiza na Deportivo Muñiz.

Tukio hilo lilitokea Novemba 12, 2026, ambapo mchezaji huyo alianguka uwanjani na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu ya dharura.

Licha ya kufanyiwa upasuaji, hali yake iliendelea kuwa mbaya na hatimaye alifariki dunia Novemba 15, baada ya siku tatu hospitalini.

Kifo chake kimeacha simanzi katika ulimwengu wa soka, hasa kutokana na umri wake mdogo na mazingira ya tukio hilo.