Manchester United itakuwa mwenyeji wa Tottenham Hotspur usiku huu wa Jumamosi, katika mchezo wa Ligi Kuu England utakaopigwa kwenye dimba la Old Trafford. Mchezo huo utaanza saa 19:30 usiku, ukiwa ni miongoni mwa michezo inayosubiriwa kwa hamu baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa.
United wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa katika nafasi ya 12 baada ya kukusanya pointi tano katika michezo mitano, wakishinda mmoja, sare mbili na kupoteza miwili. Kikosi cha Michael Carrick kinahitaji ushindi ili kuanza kupandisha kiwango na kuingia katika nafasi za juu, baada ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Fulham katika mchezo wao wa mwisho wa ligi.
Tottenham wao wanapitia wakati mgumu zaidi, wakiwa mkiani mwa msimamo wakiwa na pointi mbili pekee bila ushindi katika michezo yote mitano. Spurs wamepoteza mara tatu na kutoka sare mbili, huku wakifunga mabao mawili pekee. Hivyo, safari ya Old Trafford ni nafasi muhimu kwa kikosi cha Roberto De Zerbi kupata ushindi wao wa kwanza na kuanza kubadilisha mwenendo wa msimu.
Mchezo huo pia unatarajiwa kuwa na changamoto za upatikanaji wa wachezaji kwa pande zote mbili. United wanafuatilia hali ya Marcus Rashford, Kobbie Mainoo, Benjamin Sesko, Patrick Dorgu na Noussair Mazraoui, huku Matthijs de Ligt na Manuel Ugarte wakiwa bado nje. Tottenham nao wanawakosa baadhi ya wachezaji muhimu kutokana na majeraha, akiwemo Dejan Kulusevski, Mykhailo Mudryk, Pedro Porro, Wilson Odobert na Xavi Simons.
Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema. Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Kwa historia ya hivi karibuni, United wanaingia wakiwa na kumbukumbu nzuri baada ya kuifunga Tottenham mabao 2-0 katika mchezo wao wa mwisho Old Trafford. Hata hivyo, Spurs wamekuwa na matokeo mazuri katika baadhi ya michezo ya karibuni kati ya timu hizi.
United watategemea Bruno Fernandes na Bryan Mbeumo kuongeza nguvu katika mashambulizi, wakati Tottenham watatafuta namna ya kuvunja ukuta wa wenyeji na kuondoka Manchester na ushindi wao wa kwanza wa msimu.