Yamefungwa mabao 83 NBC Premier League 2026/27

Kivumbi kinaendelea ndani ya NBC Premier League kwa timu kusaka pointi 3 uwanjani. Nyavu zimekuwa zikitikiswa huku makipa wakiwa na jukumu kuzuia michomo kutoka kwa wapinzani.

Ni wazi kwamba mzunguko mmoja zinachezwa jumla ya mechi 8 katika viwanja tofauti huku zikirushwa mubashara Azam TV.

Ikiwa ni mzunguko wa 4 yamefungwa jumla ya mabao 83. Wastani wa mabao 20 kila mzunguko. Nyota wawili wanaongoza kufunga mabao mengi Obrey Chirwa mshambuliaji wa Geita Gold na Sopu wa Azam FC hawa kila mmoja amefuga mabao 4.

Rekodi zinaonyesha kwamba mzunguko wa 4 yamefungwa jumla ya mabao 22. Mchezo uliokusanya mabao mengi ilikuwa Singida Black Stars 4-2 Polisi Tanzania ulichezwa Uwanja wa Airtel.

Mzunguko wa 3 mabao 25 yamefungwa huu ukiwa na rekodi yakukusanya mabao mengi zaidi ndani ya msimu wa 2025/26.

Mchezo uliokusanya mabao mengi ilikuwa Geita Gold 6-2 Kagera Sugar. Ni rekodi ambayo imeandikwa kwa timu ya kwanza kupata ushindi mkubwa mbele ya mpinzani ndani ya dakika 90.

Mzunguko wa 2 yalifungwa jumla mabao 19. Mchezo uliokusanya mabao mengi ilikuwa Yanga SC 4-1 Coastal Union.

Mzunguko wa kwanza unashikilia rekodi ya kukusanya mabao kiduchu ambayo ni 17. Mchezo uliokusanya mabao mengi ilikuwa Namungo FC 1-3 Yanga SC.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Moyo Wangu Unavuja Damu na Msichana wa Maisha Yangu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Msichana wa Maisha Yangu ni simulizi mpya ambayo inazungumzia nguvu ya ahadi na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo matumizi ya AI. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.

Duniani kote kinapatikana mtandaoni bofya hapa Buy Book: Msichana wa Maisha Yangu by Lunyamadzo Mlyuka on Selar | selar.