Namungo FC vs Yanga SC

Yanga SC inayonolewa na Kocha Mkuu Manqoba Mngqithi, ilimaliza msimu wa 2025/26 ikiwa na pointi 75 baada ya mechi 30, ilipoteza mchezo mmoja pekee dhidi ya Dodoma Jiji FC.

Kwa sasa timu hiyo ipo Lindi kwa maandalizi ya mchezo wa ufunguzi ndani ya msimu mpya wa 2026/27 unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Majaliwa.

Ni Agosti 15 Namungo FC vs Yanga SC utakuwa mchezo wa kwanza kwa wababe hawa wawili kusaka pointi tatu muhimu.

Baada ya mchezo huo kete inayofuata kwao ni Yanga SC vs Coastal Union, Agosti 20, Uwanja wa Uhuru.

Yanga SC vs JKT Tanzania, Agosti 24 Uwanja wa Uhuru na Yanga SC vs Pamba Jiji FC, Agosti 28

Fountain Gate vs Simba SC, Septemba Mosi,2026 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Timu hiyo imetoka kupata ushindi kwenye mchezo uliopita dhidi ya Simba SC katika mchezo wa Ngao ya Jamii uliochezwa Uwanja wa New Amaan Complex, Agosti 12.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Moyo Wangu Unavuja Damu na Msichana wa Maisha Yangu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Msichana wa Maisha Yangu ni simulizi mpya ambayo inazungumzia nguvu ya ahadi na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo matumizi ya AI. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.