Pazia la NBC Premier League linatarajiwa kufunguliwa rasmi Agosti 14 huku Simba SC ikiwa na mechi 5 za moto mwanzo wa msimu kusaka pointi 3 muhimu.
Simba SC ilimaliza nafasi ya pili kwenye msimamo baada ya mechi 30 ikivuna pointi 73 tofauti ya pointi 2 na mabingwa Yanga SC waliomaliza msimu wakiwa na pointi 75.
Kagera Sugar iliyopanda daraja ikitokea Championship itafungua pazia kwa kumenyana na Simba SC. Mchezo huu unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Kaitaba, utapigwa Agosti 16.
Mnyama atakuwa ugenini mchezo wa pili itakuwa dhidi ya Pamba Jiji FC unatarajiwa kuchezwa Agosti 19, Uwanja wa CCM Kirumba.
Agosti 22 itakuwa ni Singida Black Stars vs Simba SC , Uwanja wa Airtel, baada ya kumenyana kwenye Kagame Cup na mnyama kushinda mabao 2-1 huu utakuwa ni mtanange kwenye ligi.
Mchezo wa kwanza kwa Simba SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Steve Barker kucheza nyumbani itakuwa dhidi ya Coastal Union, Agosti 27, Uwanja wa Uhuru. Mchezo wa tano itakuwa vs Geita Gold Uwanja wa Uhuru Agosti 31.
…
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Moyo Wangu Unavuja Damu na Msichana wa Maisha Yangu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Msichana wa Maisha Yangu ni simulizi mpya ambayo inazungumzia nguvu ya ahadi na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo matumizi ya AI. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.