Saa 18:00 jioni leo, Mei 24, Uwanja wa Tottenham Hotspur Stadium utakuwa kinara wa tamasha la kukatana shoka. Tottenham Hotspur, wanaoshika nafasi ya 17 yenye pointi 37, wanakabiliwa na hatari ya kushuka daraja la kwanza tangu 1977.
Kinyume chao, Everton iliyopo nafasi ya 10 yenye pointi 48 wana ndoto ndogo za kufuzu Kombe la Ulaya, ingawa wanategemea matokeo ya mechi nyingine. Mchezo huu una uzito tofauti kwa kila timu, kwa Spurs ni suala la kuishi, ila kwa Everton ni suala la kumaliza kwa kiwango cha juu.
Tottenham wanaingia uwanjani wakiwa na shinikizo kubwa baada ya kupoteza 1-2 kwa Chelsea, mechi ambayo ingewasaidia kujisalimisha kama wangepata angalau pointi moja. Kocha wao Roberto De Zerbi ameielezea mechi ya leo kuwa “muhimu zaidi kuliko fainali ya Europa League mwaka jana,” akisisitiza kuwa “hii ni suala la heshima na historia ya klabu”.Kwa upande mwingine, Everton wanaingia wakiwa wametulia, ingawa matumaini yao ya Ulaya yanategemea Chelsea kushindwa leo hali inayoweza kuwapunguzia motisha .
Tottenham wanakabiliwa na wimbi la majeruhi linaloogofya. Mfungaji wao Dominic Solanke, ambaye aliumia dhidi ya Wolves, ana matumaini madogo ya kucheza leo ingawa hakuwepo kwenye mechi ya Chelsea na uwezekano wake ni mdogo . Nahodha wao Cristian Romero amemaliza msimu kutokana na jeraha baya la goti lililotokea kwenye mechi ya kwanza ya De Zerbi, wakati Xavi Simons (ACL), Mohammed Kudus (hamstring), Dejan Kulusevski (goti), na Wilson Odobert (ACL) wote wamo nje. Hii inamaanisha kuwa De Zerbi anaweza kukosa hadi wachezaji wake sita muhimu katika mchezo huu wa kihistoria na maamuzi.
Ingia kwenye kasi ya kujishindia pesa kwenye michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
David Moyes anatafuta kubadilisha mbinu baada ya kupoteza 3-1 kwa Sunderland wiki iliyopita. Jake O’Brien anayetarajiwa kuondolewa kwenye kikosi, na James Garner anaweza kuhamia beki ya kulia huku Merlin Rohl akijaza kiungo cha kati. Beto anaendelea kuwa hatari kikubwa mbele, wakati Iliman Ndiaye anatafuta kurudi kwenye kiwango chake baada ya kukosa mabao kwa wiki kadhaa. Kipa Jordan Pickford, ambaye alikuwa kwenye kiwango kizuri kwenye mechi ya awali dhidi ya Spurs msimu huu (ushindi wa 3-2 kwa Everton Oktoba 2025), atakuwa muhimu.
Kwa mujibu wa head-to-head, Tottenham wana rekodi nzuri dhidi ya Everton kwa ujumla, lakini katika msimu huu wamepoteza 2-3 ugenini na kushinda 3-0 nyumbani . Nafasi ya Tottenham ya kusalimu amri iko mikononi mwao: pointi moja inatosha kwa sababu ya tofauti yao nzuri ya mabao dhidi ya West Ham United. Lakini kwa kukosa wachezaji wao muhimu na kiwango cha chini cha ujasiri (hawajashinda ligi nyumbani tangu Desemba), wako katika hatari. Everton wana nguvu zaidi kwenye karatasi, lakini Spurs watapambana kwa uhai wao wenyewe.