FT: TRA United 0-0 Simba SC

Ubao wa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid umesoma TRA United 0-0 Simba SC. Umiliki wa mpira ilikuwa ni asilimia 39 kwa wenyeji na wageni asilimia 61.

Huu ni mchezo wa mzunguko wa kwanza ambao ulikuwa ni kiporo baada ya mwanzo mchezo huu kuahirishwa kutokana na mvua kubwa kunyeshwa.

Matokeo hayo yanaifanya Simba SC kufikisha jumla ya pointi 36 kwenye msimamo ikiwa nafasi ya pili huku vinara wakiwa ni Yanga SC wenye pointi 44.

TRA United nafasi ya 7 ikiwa na pointi 24 baada ya kucheza mechi 18 msimu wa 2025/26.

Mchezaji Valentino Nouma wa TRA United alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano kipindi cha pili dakika ya 82 na 87.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.