UBAO wa Tanzanite Kwaraa, Manyara umesoma Mbeya City 0-0 Azam FC NBC Premier League leo Aprili 9, 2026.
Wababe hawa wawili wamekamilisha dakika 90 bila kufungana kwenye mchezo wa leo uliokuwa na ushindani mkubwa ndani ya uwanja.
Matokeo hayo yanaifanya Mbeya City kufikisha jumla ya pointi 17 ikiwa nafasi ya 12 huku Azam FC nafasi ya 3 na pointi 34 ikiwa imecheza mechi 18.
Pemba Kelvin amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo wa leo mbele ya matajiri wa Dar, Azam FC ambao bado hawajapoteza ndani ya ligi.
Katika mchezo wa leo ni mashuti 9 Azam FC walipiga kuelekea lango la wapinzani huku wapinzani wakipiga jumla ya mashuti 3.
Mchezo uliopita Azam FC iligawana pointi moja dhidi ya Simba SC ikiwa nyumbani, Uwanja wa Azam Complex na mchezaji bora alikuwa ni Aishi Manula ambaye alianza langoni mchezo wa leo.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.