Dakika 90 zimekamilika kwenye mchezo wa leo huku ubao ukisoma Pamba Jiji FC 0-3 Yanga SC, Aprili 8, 2026 kwenye NBC Premier League, Uwanja wa CCM Kirumba.
Magoli ya Yanga SC yamefungwa na Mudathir Yahya dakika ya 8 na 34 huku goli la tatu likifungwa na Maxi Nzengeli dakika ya 66 ya mchezo.
Ni Allan Okello kiungo wa Yanga SC ametoa pasi zote zilizoleta magoli ikiwa ni pointi tatu nyingine muhimu kwa mabingwa watetezi.
Yanga SC anafikisha pointi 44 kwenye msimamo wa ligi baada ya mechi 18 akijikita kileleni katika msimamo na Pamba Jiji FC anashushwa kutoka nafasi ya 5 mpaka ya 6.
Pointi zake ni 26 baada ya mechi 18 ndani ya msimu wa 2025/26.
Mechi zote mbili Yanga SC mbele ya Pamba Jiji FC amepata ushindi wa magoli 3-0.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.