TDS U17 vs Fountain Gate kukipiga fainali mashindano ya kusaka vipaji

Fountain Gate Academy ya Morogoro imetinga hatua ya fainali katika mashindano ya kusaka vipaji yaliyofanyika Viwanja vya TFF Center, Kigamboni.

Ni TDS U17 vs Fountain Gate watakutana katika mchezo wa fainali kusaka bingwa baada ya kukata tiketi yakutinga kwenye hatua hiyo.

Mashindano hayo ambayo yameongezewa nguvu na EMWANI fainali yake inatarajiwa kuchezwa kesho, Machi 29, 2026, Uwanja wa KMC, Complex.

Mashindano hayo yamekuwa na mwamko mkubwa kwa timu za watoto kujiandikisha na kushiriki katika kuibua vipaji.

Kila timu imekuwa ikionyesha ushindani jambo ambalo linaongeza ugumu kwenye fainali hiyo inayotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Mashindano hayo yamefunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Yanga SC, Arafat ambaye alibainisha kuwa malengo ni kuona vipaji vinaendelezwa zaidi katika kufanikisha ndoto za kila mwenye uwezo.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.