Mechi za Kombe la Dunia Kufutwa Gillette Stadium Kwa Kukosa Fedha za Ulinzi

Mechi za FIFA World Cup zilizopangwa kuchezwa katika Gillette Stadium huenda zikafutwa iwapo mamlaka za eneo hilo hazitapokea fedha za kutosha kwa ajili ya ulinzi wa mashindano.

Uwanja huo  ambao ni nyumbani kwa timu ya NFL New England Patriots unatarajiwa kuwa mwenyeji wa jumla ya mechi saba, ikiwemo pambano la England dhidi ya Ghana Juni 23. Hata hivyo, changamoto ya gharama za usalama imeibua mjadala mkubwa.

💰 Mzozo wa Pauni Milioni 6

Viongozi wa mji wa Foxborough wanataka FIFA ichangie kiasi cha pauni milioni 6 ili kugharamia askari, miundombinu na ulinzi kwa kipindi cha siku 39 za mashindano.

Mjumbe wa bodi ya mji huo, Bill Yukna, amesema:

“Ni sawa na kuandaa Super Bowl saba hapa. Tunatakiwa kuulinda uwanja kwa siku 39 mfululizo, jambo ambalo si dogo.”

Alisisitiza kuwa lengo lao si kuzuia mashindano bali ni kuhakikisha usalama wa wakazi wao unalindwa.

🏘️ “Sisi Ni Mji Mdogo”

Mjumbe mwingine, Stephanie McGowan, amesema Foxborough ni mji mdogo wenye wakazi wapatao 18,000 pekee, hivyo hauna rasilimali za kutosha kubeba mzigo huo peke yake.

Mashindano yanatarajiwa kuanza rasmi Juni 11, na sasa macho yote yanaelekezwa kuona kama makubaliano ya kifedha yatafikiwa kwa wakati ili kuepusha kufutwa kwa mechi hizo.