Simba SC 3-0 Greenland FC matokeo ya dakika 90 mchezo wa CRDB Federation Cup hatua ya 64 bora Uwanja wa Mej Isahmuyo.
Magoli ya Simba SC yamefungwa na Baraka Mwangosi dakika ya 13, Anthony Mligo dakika ya 45 na kamba ya tatu imefungwa na Neo Maema dakika ya 90.
Mwangosi amefunga goli hilo akitumia makosa ya mlinda mlango wa Greenland FC ambaye katika harakati za kuokoa hatari mpira wake ulikutana na mpinzani akiwa ndani ya 18.
Mligo alifunga goli la pili ikiwa ni sekunde chache kabla ya mapumziko na Maema aliyeanzia benchi alifunga goli la 3 muda mfupi kabla ya mpira kufika tamati.
Ushindi huo unawafungashia virago Greenland FC huku mnyama akisonga mbele hatua ya 32 bora.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.