Kiwango mastaa Yanga SC chamkosha kocha

KIWANGO cha mastaa wa Yanga SC walichoonesha mchezo wa mwisho hatua ya makundi vs JS Kabylie kimemkosha Kocha Mkuu Pedro Goncalves kwa kubainisha kwamba wachezaji walijituma bila kuchoka.

Katika mchezo huo wa makundi uliochezwa New Amaan Complex, Februari 15 2026 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga SC 3-0 JS Kabylie ukiwa ni ushindi mkubwa waliofunga nao kwenye makundi.

Yanga SC imemaliza hatua ya makundi ikiwa na pointi 8 nafasi ya 3 huku Al Ahly na AS Far Rabat kutoka kundi B zikitinga hatua ya robo fainali.

Pedro amesema walitumia nguvu kubwa na akili kwenye mchezo huo kutafuta matokeo jambo ambalo lilifanikiwa licha yakushindwa kusonga mbele.

“Wachezaji wamefanya kazi kubwa kutafuta matokeo kwenye mchezo wetu wa mwisho na ilikuwa hivyo. Kwa kila namna ninawapongeza kwa kuwa walifanya kazi kubwa.

“Kushindwa kusonga mbele haikuwa mpango wetu ila tuna kazi kuelekea msimu ujao kuwa imara kwenye mashindano ya kimataifa,”.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.