Meridianbet Yajivunia Miradi Zaidi 500 Ya Ustawi wa Jamii

Katika hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na American Chamber of Commerce (AmCham), Meridianbet ilisimama kifua mbele kama mmoja wa washiriki wakuu, ikiweka bayana mafanikio yake katika eneo la uwajibikaji kwa jamii. Tangu mwaka 2009, kampuni hiyo imetekeleza miradi zaidi ya 500 ya kijamii nchini, hatua inayoonyesha kwa vitendo dhamira yake ya kurudisha kwa jamii inayoiunga mkono.

Miradi hiyo imegusa sekta nyeti kwa maendeleo ya taifa. Kuanzia programu za elimu, mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana na wafanyabiashara wadogo, hadi udhamini wa michezo ya vijana na kampeni za afya ya umma. Aidha, miradi ya kuboresha miundombinu ya kijamii imepewa kipaumbele, ikilenga kuleta mabadiliko endelevu na yanayoonekana katika maisha ya wananchi.

Meridianbet haikuachi nyuma, kuna michezo mbalimbali ya kasino mtandaoni pamoja na mechi za kimataifa za kubashiri zenye odds bomba zinazokuongezea nafasi ya kuongeza kipato chako kila siku. Kujiunga ni rahisi, Tembelea meridianbet.co.tz au piga *149*10#.

Kama sehemu ya Golden Matrix Group (NASDAQ: GMGI), Meridianbet Tanzania inanufaika na uzoefu wa kimataifa katika kuendesha biashara kwa uwazi na uwajibikaji. Katika sekta ya michezo ya kubahatisha ambayo mara nyingi hukosolewa kwa kutanguliza faida, Meridianbet imejijengea taswira tofauti kwa kuchagua kujenga, kushirikisha na kurejesha kwa jamii kwa zaidi ya miaka 17.

Uwajibikaji huo unaimarishwa na sera madhubuti za ulinzi wa wateja. Kampuni imeweka mifumo ya kubaini mapema mienendo hatarishi, kutoa huduma kwa wateja kwa usahihi na uharaka, pamoja na kuweka mipaka ya matumizi ili kuhakikisha burudani inabaki kuwa salama na yenye uwiano.

Zaidi ya hayo, Meridianbet imeanzisha mtandao wa mabalozi wa jamii unaowawezesha wateja kushiriki moja kwa moja katika miradi ya uwajibikaji kwa jamii (CSR). Ikiungwa mkono na zaidi ya wafanyakazi 200 na mamia ya washirika wa rejareja kote nchini, kampuni imeweka wazi msimamo wake wa kuiona Tanzania si soko la muda mfupi, bali kitovu cha uwekezaji wa muda mrefu na ushirikiano wa kudumu.