LIGI ya Mabingwa Afrika CAFCL inaendelea tena leo Februari 15, 2026 kwa mechi mbili za kuhitimisha hatua ya makundi huku wawakilishi wa Tanzania waliosalia kwenye michuano hiyo, Young Africans Sc wakitupa karata yao ya mwisho ya kuwania kufuzu robo fainali.
Wananchi (pointi 5) wapo nyumbani, New Amaan Complex Zanzibar kuchuana na washika mkia wa kundi B, JS Kabylie (pointi 3) huku vinara wa kundi hilo, Al Ahly (pointi 9) wakiwa wenyeji wa FAR Rabat (pointi 8)
Yanga Sc wanahitaji ushindi mnono dhidi ya JS Kabylie wakati huo wakielekeza dua zao Cairo International kuiombea Al Ahly ipate ushindi mnono dhidi ya FAR Rabat ili wafuzu.
Matokeo mengine tofauti na ushindi kwa Al Ahly yataiondosha Yanga Sc kwenye mashindano hata kama watapata ushindi wowote dhidi ya JS Kabylie.
⌚ 19:00 Yanga Sc 🇹🇿 🆚 🇩🇿 JS Kabylie
🏟️ New Amaan Complex, Zanzibar
⌚ 19:00 Al Ahly 🇪🇬 🆚 🇲🇦 FAR Rabat
🏟️ Cairo International Stadium
MSIMAMO KUNDI B kwenye mabano (magoli ya kufunga na magoli ya kufungwa)
1.🇪🇬 Al Ahly – pointi 9 (8-3)
2.🇲🇦 FAR Rabat – pointi 8 (3-2)
3.🇹🇿 Yanga Sc – pointi 5 (2-4)
4.🇩🇿 JS Kabylie – pointi 3 (1-5)