Katika kuendeleza falsafa ya kugusa maisha ya wananchi kwa vitendo, Meridianbet imeandaa zoezi maalum la msaada wa kijamii lililofanyika wilayani Kinondoni, Dar es Salaam. Kupitia mpango huu, familia zinazokabiliwa na changamoto za kiuchumi zilipatiwa msaada uliolenga kupunguza mzigo wa maisha na kurejesha matumaini mapya.
Zoezi hilo lilijikita katika utoaji wa vyakula na bidhaa muhimu za matumizi ya nyumbani, hatua iliyolenga kuimarisha upatikanaji wa chakula kwa kaya zilizo katika mazingira magumu. Mpango huu ni sehemu ya mkakati mpana wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) wa Meridianbet, unaolenga kutoa msaada wenye athari ya moja kwa moja kwa ustawi wa familia.

Mwakilishi wa Meridianbet, Nancy Ingram, alieleza kuwa kampuni imejipambanua kwa kuunganisha mafanikio ya biashara na ustawi wa jamii. Alisisitiza kuwa Meridianbet itaendelea kusimama bega kwa bega na wananchi kwa kutekeleza miradi inayotoa suluhisho la kweli kwa changamoto za kijamii.
Meridianbet haikuachi nyuma, kuna michezo mbalimbali ya kasino mtandaoni pamoja na mechi za kimataifa za kubashiri zenye odds bomba zinazokuongezea nafasi ya kuongeza kipato chako kila siku. Kujiunga ni rahisi! Tembelea meridianbet.co.tz au piga *149*10#.
Kwa wanufaika, msaada huu umeleta faraja na kuonesha kuwa bado kuna wadau wanaojali ustawi wa jamii. Meridianbet imeahidi kuendelea kuwekeza katika miradi ya kijamii ikiwemo afya, elimu, mazingira na msaada kwa makundi maalum, ikiwa ni sehemu ya safari yake ya kujenga jamii imara na yenye matumaini ya muda mrefu.