Meridianbet imechagua kuuangalia usafi wa mazingira kama nguzo muhimu ya maendeleo ya jamii. Kupitia ushiriki wake katika shughuli za usafi Kata ya Mbezi Juu, kampuni hiyo imelenga kuonesha kuwa mazingira safi yana mchango mkubwa katika kuboresha afya, tija ya wananchi na ustawi wa kijamii kwa ujumla.
Meridianbet ililenga kuwawezesha wananchi kwa vitendo. Kampuni hiyo ilitoa vifaa mbalimbali vya usafi ikiwemo mifagio, mafyekeo, koleo, glovu, mifuko ya taka pamoja na viatu vya kazi, pamoja na kushiriki bega kwa bega kwenye tukio hilo, hatua iliyolenga kuhakikisha shughuli za usafi zinaendelea kwa mpangilio na kwa usalama hata baada ya zoezi rasmi kukamilika.
Mwakilishi wa Meridianbet, Nancy Ingram, alieleza kuwa kampuni inaamini kuwa hatua bora ya kulinda afya ya jamii huanza na mazingira safi. Alifafanua kuwa magonjwa mengi ya mlipuko hutokana na uchafu na mifumo duni ya usimamizi wa taka, hivyo Meridianbet ikaona umuhimu wa kushiriki kuchukua hatua za mapema za kuzuia madhara hayo.
Meridianbet haikuachi nyuma, kuna michezo mbalimbali ya kasino mtandaoni pamoja na mechi za kimataifa za kubashiri zenye odds bomba zinazokuongezea nafasi ya kuongeza kipato chako kila siku. Kujiunga ni rahisi! Tembelea meridianbet.co.tz au piga *149*10#.
Diwani wa Kata ya Mbezi Juu aliipongeza Meridianbet kwa kushirikiana kwa karibu na serikali za mitaa, akisisitiza kuwa maendeleo ya kweli hupatikana pale ambapo sekta binafsi na uongozi wa serikali wanaposhirikiana. Ushirikiano huu ulitajwa kuwa mfano bora wa jinsi wadau tofauti wanavyoweza kuunganisha nguvu kwa lengo la pamoja la kulinda afya ya wananchi.
Kupitia tukio hili, Meridianbet imeweka bayana kuwa itaendelea kuwekeza katika miradi ya kijamii yenye athari za muda mrefu. Kampuni hiyo imesisitiza kuwa usafi wa mazingira ni jukumu la pamoja na itaendelea kuwa mshirika wa karibu wa jamii katika kuhakikisha mazingira yanabaki kuwa salama, safi na rafiki kwa maendeleo ya sasa na ya baadaye.