Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2025 imepata fainali yake baada ya Morocco na Senegal kufanikiwa kuvuka hatua ya Nusu Fainali.
Morocco walikata tiketi ya Fainali baada ya kuitoa Nigeria kwa mikwaju ya penalti kufuatia sare tasa ya 0-0 ndani ya dakika 90 za kawaida na dakika 30 za nyongeza. Katika hatua ya penalti, Morocco walishinda kwa mikwaju 4-2, na kuendeleza ndoto yao ya kulitwaa taji hilo.
Kwa upande wa pili, Senegal walithibitisha ubora wao baada ya kuiondoa Egypt kwa ushindi wa bao 1-0, likifungwa na nyota wao Sadio ManΓ©. Ushindi huo umeifanya Senegal kufuzu Fainali ya AFCON kwa mara ya tatu ndani ya matoleo manne ya mwisho, rekodi inayodhihirisha uimara wao barani Afrika.
Kwa sasa macho yote yanaelekezwa kwenye Fainali ya AFCON 2025, ambapo Simba wa Milima ya Teranga Senegal watakutana na Simba wa Atlas wa Morocco, katika pambano linalotarajiwa kuwa kali na la kusisimua.
Morocco π²π¦ π Senegal πΈπ³
ποΈ Jumapili, Januari 18, 2026
ποΈ Stade Prince Moulay Abdallah (Rabat)
Capacity: 69,500
Nani atabeba ubingwa?