Rais Samia Suluhu Hassan amezitaka mamlaka zote zinazohusika na michezo, kuhakikisha wachezaji wa Kitanzania wanaandaliwa katika mazingira bora ili waliwakilishe vyema taifa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanaboreshewa posho zao.
Rais Samia amesimulia jinsi alivyopokea taarifa za wachezaji wa Taifa Stars kugoma kwenda Morocco kutokea nchini Misri kwa sababu ya kudai posho zao.
Ameyasema hayo katika hafla ya kuipongeza Timu ya Taifa, Taifa Stars iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam na kuenda sambamba na hafla ya kuwapongeza wanamichezo wote waliofanya vizuri katika michuano ya kimataifa na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania.