JUMAPILI yenye utulivu imeshuhudia moja ya mchezo wenye ushindani mkubwa na dakika 90 zikikamilika kwa mabao 5 kufungwa uwanjani.
Gabon 2-3 Msumbiji mchezo wa hatua ya makundi AFCON 2025 nchini Morocco Desemba 28,2025. Ni mchezo wa pili kati ya mitatu kwa kundi F.
Magoli ya Gabon yamefungwa na Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya 45+5 na Moucketou-Moussounda dakika ya 76.
Kwa upande wa Msumbiji ni Faisal Bangal dakika ya 37, Geny Catamo dakika ya 42 kwa mkwaju wa penalti na Diogo Calila dakika ya 52.
Matokeo haya yanaifanya Gabon kusalia nafasi ya nne ikiwa haijakudanya pointi huku Msumbiji ikiwa nafasi ya tatu na pointi tatu.
Vinara kwenye kundi ni Ivory Coast na Cameroon nafasi ya pili zote zikiwa na pointi tatu kibindoni.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.