Bayern Yaamka na Kupindua Meza, Yapiga Sporting 3-1 UCL
Bayern Munich imeonyesha ubabe katika dimba la Allianz Arena baada ya kutoka nyuma 1-0 na kuibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Sporting Lisbon kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kichekesho kilitokea dakika ya 54 baada ya Joshua Kimmich kujifunga na kuwapa Sporting uongozi, lakini Bayern ikarejea mchezoni kwa nguvu na kufunga mabao matatu…